Owalo aongoza upanzi wa miche 10,000 Maseno

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Mkuu wa utumishi wa umma Eliud Owalo, aongoza upanzi wa miche 10,000 Maseno.

Naibu Mkuu wa Utumishi wa Umma Eliud Owalo leo Jumamosi alishirikiana na wanafunzi na walimu na maafisa wengine wa shule ya Maseno katika upanzi wa miche 10,000.

Kulingana na Owalo, zoezi hilo linaambatana na mpango wa serikali wa upanzi wa miti bilioni 15 kwa lengo la kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Owalo alitoa wito kwa wadau wote kaunti ya Kisumu, kuimarisha juhudi za upanzi wa miti, ili kuafikia asilimia 10 ya utandu wa mistu hapa nchini.

Serikali ya Rais William Ruto, inalenga upanzi wa wa miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Mnamo Jumatatu Novemba 4,2024, katibu katika wizara ya usalama wa taifa atazindua mpango unaoongozwa na machifu wa kutenga siku ya kutekeleza hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi.

Kila Jumatatu ya kwanza ya kila mwezi, Machifu watatakiwa kushirikiana na jamii katika upanzi wa miti na utoaji mafunzo kuhusu utunzaji wa mazingira.

Share This Article