Odira, Moraa, Oketch, na Were wawahi tiketi za Dunia

Oketch amevunja rekodi ya kitaifa ya sekunde 50.38 iiyoandikishwa mwaka 2023 na Mary Moraa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Lillian Odira, Sarah Moraa, Mercy Oketch na Wiseman Were Mukhobe, wamefuzu kwa mashindano ya Riadha Duniani mwezi Septemba mwaka huu baada ya kutamba katika mbio za Kip Keino Classic Continental Tour, leo.

Odira aliongoza mbio za mita 800 katika Makala ya sita ya mbio za Kip Keino Classic continental tour Jumamosi jioni kwa muda wa dakika 1 sekunde 58.31.

Oratile Nowe wa Botswana alimaliza wa pili kwa dakika 1 sekunde 58.47 huku bingwa wa Afrika, Sarah Moraa, akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 1 sekunde 58.96 na pia kufuzu kwa mashindano ya dunia.

Mercy Oketch amejikatia tiketi kwa mashindano ya Dunia katika mita 400 akiweka rekodi mpya ya kitaifa ya sekunde 50.14 .

Oketch amevunja rekodi ya kitaifa ya sekunde 50.38 iiyoandikishwa mwaka 2023 na Mary Moraa.

Wiseman alishinda mbio za mita 400 kwa sekunde 48.38 akijikatia tiketi kwa mashindano ya riadha duniani ya Tokyo, Japan, Septemba mwaka huu.

Website |  + posts
Share This Article