Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR) Roseline Odede atazikwa Januari 18 kijijini Ruma, kaunti ya Siaya.
Familia ya marehemu hata hivyo imesema itatoa taarifa zaidi za mipango ya mazishi baadaye.
Odede alifariki Januari 3 mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehemu alikuwa mkewe Dkt. Joram Odede na amewaacha watoto wawili, Clara Odede na Diane Odede.
Hadi kifo cahke, Odede alikuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na mpatanishi.