NTSA: Nambari mpya za usajili wa magari ziko tayari

Tom Mathinji
1 Min Read

Halmashauri ya uchukuzi na usalama barabarani  (NTSA), imetoa wito kwa wenye magari ambao wamepokea ujumbe mfupi, kuchukua nambari za usajili wa magari.

Hatua hiyo inajiri baada ya halmashauri hiyo kuongeza muda wa kufanya kazi kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.

Mabadiliko hayo yaliyotangazwa na Mkurugenzi mkuu wa halmashauri hiyo, yalitokana na agizo lililotolewa na Waziri wa uchukuzi na barabara  Kipchumba Murkomen, lililotaka halmashauri hiyo kukamilishwa mrundiko wa uchapishaji leseni za kuendesha magari, vyeti vya kumiliki gari na nambari za usajili wa magari katika muda wa wiki mbili.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya ghafla katika afisi za NTSA Jijini Nairobi, waziri Murkomen  alisikitika kuwa zaidi ya maombi 50,000 ya leseni za kuendesha gari, zilitumwa mwezi Septemba mwaka jana, na bado hazikuwa zimechapishwa.

Share This Article