Nitarejesha hadhi ya IEBC, asema Nyachae

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwaniaji Uenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini IEBC, Charles Nyachae, amesema atarejesha hadhi ya taasisi hiyo endapo atateuliwa mwenyekiti mpya.

Nyachae amesema haya alipofika mbele ya jopo la usaili, akiongeza kuwa licha ya Mahakama ya Upeo kuthibitisha kuwa uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2022, uliafiki viwango vya ubora kikatiba, hilo halitoshi kumhakikishia mwananchi utendakazi wa IEBC.

Aidha, Nyachae amesema hatajiuzulu akipata shinikizo katika IEBC alivyofanya akiwa Jaji wa mahakama ya Kisheria ya Afrika Mashariki mwaka jana.

Nyachae, ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa tume ya utekelezaji wa katiba CIC, amekanusha madai ya kupendelewa na serikali katika mahojiano kwa kazi hiyo.

Mahojiano hayo ambayo yameanza leo yatakamilika Jumatato hii, huku mwenyekiti mpya wa IEBC akitarajiwa kutangazwa mwezi ujao.

Nyachae alikuwa  msaili wa tatu  na wa mwisho wa leo ,baada ya Abdulqadir Lorot na Anne Amadi.

Website |  + posts
Share This Article