Waziri wa michezo Kipchumba Murkone ameliambia bunge la taifa kwamba Rais anayeondoka wa shiriko la soka nchini FKF, hajastahiki kuwa naibu wa Dorris Petra katika chaguzi zijazo za shirikisho hilo.
“Sheria zinamzuia Mwendwa kuwa naibu wa mwaniaji yeyote katika uchaguzi huo utakaoandaliwa Disemba 7,2024, kwa sababu amekamilisha muhula wake afisini,” aliambia kamati ya bunge kuhusu michezo wakati wa mkutano katika jengo la bunge leo Jumanne.
Aidha waziri huyo aliongeza kuwa:”Ni utovu wa maadili kuhudumu kama Rais wa shirikisho hilo, tena kujiwasilisha kama naibu Rais”.
Murkomen aliongeza kuwa wizara yake inajitahidi kuhakikisha chaguzi hizo zinafanyika kwa njia huru na wazi.
Kulingana na waziri huyo, miongoni mwa hatua alizochukua ni pamoja na kuhamisha afisi za bodi ya uchaguzi ya FKF kutoka jumba la Kandanda hadi katika eneo ambalo lisiloegemea upande wowote.