Ni kufa kupona kundini B mechi za mwisho Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read

Kivumbi kinatarajiwa kutifuliwa katika mechi za mwisho za kundi B katika kipute cha CECAFA kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18.

Mechi za kundi B zitakamilika Jumamosi Zanzibar, Tanzania, Uganda na Sudan Kusini zikiwa na pointi tatu kila moja.

Uganda watamenyana na Sudan Kusini katika uwanja wa Mamboleo katika kaunti ya Kisumu wakati Tanzania wakimaliza udhia na ndugu zao Zanzibar.

Mechi za nusu fainali zitaandaliwa Jumanne ijayo huku fainali ikipigwa Ijumaa ijayo.

Timu mbili bora kundini B zitajiunga na Kenya na Rwanda ambao tayari wamefuzu kwa nusu fainali kutoka kundi A.

Share This Article