Nairobi United FC wajikaza kisabuni na kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho

Dismas Otuke
2 Min Read

Klabu ya Nairobi United inayofadhiliwa na kaunti ya Jiji la Nairobi iliandikisha historia Jumapili baada ya kuwashinda wenyeji Etoile Du Sahel ya Tunisia , penati 7-6, kufuatia sare ya 2-2 baada ya mikondo miwili.

Nairobi United, inayofunzwa na mchezaji wa zamani Nicholas Muyoti, ilikuwa imeshinda duru ya kwanza katika uwanja wa Nyayo kwa mabao 2-0, na kisha wakalemewa 2-0 ugenini mjini Sousse, Tunisia, katika mechi ya marudio jana.

Kipa wa United Kevin Oduor alikuwa shujaa wa  mechi akipangua penati ya kwanza ya nahodha Nahim Nhid na pia mkwaju wa mwisho wa saba wa Tunisia uliochongwa na Cedric Gbo.

John Otieno, Brian Mzee, Kevin Otiende, Lennox Ogutu, Chris Opondo , Brian Magare  na Kevin Oduor ,walifunga penati za Nairobi United.

Timu hiyo iliyoshinda la Mozart msimu jana na kupandishwa ngazi kushiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ndiyo timu ya kwanza ya Kenya kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe hilo tangu Gor Mahia, waliposhiriki msimu wa mwaka 2018/2019.

Naiboi wanavyojulikana watapokea takriban shilingi milioni milioni 6.4 kutoka kwa shirikisho la soka Afrika CAF kwa kufikia hatua hiyo ya mchujo .

Aidha, ni afueni kwa Nairobi United ambao watapokea takriban shilingi milioni 51.6, endapo watamaliza katika nafasi ya tatu au nne katika hatua ya makundi na milioni 71 ikiwa watafuzu kwa robo fainali ya kombe hilo.

Website |  + posts
Share This Article