NACADA yaharibu lita 29,000 za pombe haramu Kiambu

Operesheni hiyo pia iliwezesha kuharibiwa kwa vifaa vinavyotumiwa kutenegeneza pombe haramu, kwa kuzingatia taratibu za kisheria.

Tom Mathinji
1 Min Read
NACADA yaharibu lita 29,000 ya pombe haramu Kiambu

Halmashauri ya Kitafa ya Kupambana na Mihadari na Pombe Haramu (NACADA), imetekeleza operesheni ya kijasusi na kuharibu lita 29,240 za pombe haramu katika eneo la Soweto, Kahawa West, Kaunti ya Kiambu.

Operesheni hiyo pia iliwezesha kuharibiwa kwa vifaa vinavyotumiwa kutenegeneza pombe haramu, kwa kuzingatia taratibu za kisheria.

Wakati wa operesheni hiyo, mwanamume mmoja alikamatwa na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kasarani akisubiri kufikishwa mahakamani.

Kufuatia msako huo, Afisa Mkuu Mtendaji wa NACADA Dkt.  Anthony Omerikwa aliwapongeza maafisa waliotekeleza operesheni hiyo, akikariri kujitolea kwa halmashauri hiyo kukabiliana na pombe haramu katika jamii na kulinda afya ya umma.

“Operesheni hii ni ishara kamili kwamba  NACADA haitalegeza kamba kwenye vita dhidi ya pombe haramu na bidhaa zingine hatari,” alisema Omerikwa.

Share This Article