Mshukiwa wa wizi uliotekelezwa Parklands akamatwa

Mshukiwa huyo Obed Makori, alikamatwa kwenye barabara ya Northern Bypass na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Gigiri.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa wizi akamatwa Nairobi.

Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), wamemkamata mshukiwa aliyenaswa kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, akimuibia mtu mali yake katika mtaa wa Parklands kabla ya kutoroka.

Mshukiwa huyo Obed Makori, alikamatwa kwenye barabara ya Northern Bypass na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Gigiri.

Wakati wa wizi huo, mshukiwa huyo aliangusha bastola, ambayo ilichukuliwa na polisi na kuhifdhiwa kama ushahidi.

Aidha, mshukiwa huyo alienda mafichoni baada ya kutekeleza uhalifu huo, huku akikwepa mitego ya polisi, hadi alipokamatwa kwenye operesheni hiyo iliyotekelezwa na polisi.

Kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa kwenye  korokoro za polisi, akisubiri kufikishwa mahakamani, huku polisi wakiendeleza operesheni kumtafuta mshirika wake aliye mafichoni.

TAGGED:
Share This Article