Mzozo wa Kidiplomasia unanukia baina ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya Congo kushitaki Kigali kwa mahakama ya afrika mashariki yenye makao yake mjini Arusha.
Kwenye kesi hiyo iliyowasilishwa mwaka uliopita lakini ikafanyiwa marekebisho mwaka huu Congo wanaishitaki Rwanda kwa kuchochea vita nchini Congo kinyume na sheria za kimataifa.
Mahakama ya Afrika mashariki inatarajiwa kusikiza na kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo.
Congo wamekuwa wakiishutumu majirani Rwanda kwa kuchangia vita kwa kuunga mkono makundi ya upinzani