Mwili wa afisa wa polisi wa Kenya aliyefariki Haiti wawasili nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwili wa afisa wa polisi wa Kenya aliyefariki nchini Haiti wawasili hapa nchini.

Mwili wa afisa wa polisi wa Kenya aliyefariki nchini Haiti uliwasili nchini jana Jumatatu jioni.

Samuel Tompoi Kaetuai, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha kimataifa  cha kusaidia kudumisha usalama nchini Haiti kinachoongozwa na Kenya, aliuawa mwezi uliopita alipokuwa akishika doria.

Mwili huo ulipokelewa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta – JKIA.

Wiki iliyopita, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja pamoja na maafisa wengine wakuu wa serikali waliitembelea na kuifariji familia ya afisa huyo katika kijiji cha Naserian, kaunti Ndogo ya Kajiado Mashariki, kaunti ya Kajiado.

Mwili huo baadaye ulipelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Chiromo huku mipango ya mazishi ikiendelea.

Website |  + posts
Share This Article