Mwijaku amedai kwamba mrembo Zuchu tayari ameandika barua ya kuomba kuondoka kwenye kampuni inayomsimamia ya WCB inayoendeshwa na mume wake Diamond Platnumz.
Mwanamitandao huyo alisema hayo katika mahojiano na wanahabari kuhusu kufungiwa nyumba ambapo mwanahabari alimuuliza kuhusu iwapo siku moja Zuchu ataondoka WCB.
“Sio siku moja, tushaandika barua, barua ishaandikwa. Wakatae nitoe nakala, wakikataa natoa nakala,” alijibu Mwijaku akiongeza kwamba Zuchu anasubiri majibu.
Alipoulizwa kuhusu hela nyingi ambazo huenda akaitishwa kabla ya kukubaliwa kugura WCB, Mwijaku alisema kwamba watachangisha hela hizo na yeye atakuwa wa kwanza kutoa mchango.
Katika mahojiano hayo Mwijaku alisisitiza kwamba maelezo yake kuhusu kilichomfanya Zuchu atangaze kutengana na Diamond ndiyo ya kweli.
Zuchu aliwahi kuandika kwenye Instagram kwamba yeye na Diamond wameachana na tayari ameanzisha taratibu za talaka.
Tangazo hilo lilijiri muda mfupi baada ya sherehe iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mamake Diamond ambayo yeye hakuhudhuria.
Kwenye sherehe hiyo Diamond alimwita mtangazaji wa Wasafi Fm Aaliyah kwa madaha akitumia kipaaza sauti huku akimtaka afike mbele kwa ajili ya kumpa mama Diamond Zawadi.
Wakati huo Mwijaku alisema kwamba Diamond alimdhalilisha mkewe Zuchu kwa kumwonyesha mtangazaji huyo heshima na upendo uliopitiliza akimrejelea kuwa hawara wake.
Anasema siku hiyo Zuchu alimpigia simu akilia naye akamshauri kufanya dua na sasa yuko sawa, ana mtoto na ana furaha.