DCI yachunguza mauaji tatanishi ya Dkt. Mutiso

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI inasema Dkt. Mutiso alikumbana na mauti katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi Julai 29, 2026 asubuhi. 

Martin Mwanje
1 Min Read
Dkt. Victoria Nthunya Mutiso aliyepigwa risasi na kuuawa Julai 29, 2026

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI inasema inachunguza kisa cha kufyatuliwa risasi hadi kufariki kwa Dkt. Victoria Nthunya Mutiso kilichotokea leo Jumatano asubuhi. 

DCI inasema Dkt. Mutiso alikumbana na mauti katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi.

“Punde baada ya kupokea ripoti, maafisa wa polisi, wakisaidiwa na makachero wa Uhalifu wa Eneo la Tukio (CSI), walizuru haraka, na kuchukua ushahidi katika eneo la tukio,” ilisema DCI kwenye taarifa wakati ikiomboleza familia ya marehemu.

“Ushahidi husika wa kisayansi ulichukuliwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya uchambuzi, huku  mashahidi wakihojiwa kama sehemu ya upelelezi unaoendelea.”

DCI ikisema makachero pia walitembelea hospitali ambako marehemu alikimbizwa kwa matibabu kabla ya kukumbana na mauti.

Upelelezi wa awali unaashiria kuwa Dkt. Mutiso alikuwa ameitisha teksi ya Uber alipofyatuliwa risasi na kujeruhiwa hadi kufariki katika mazingira ambayo ni ya kutatanisha.

Makachero wa mauaji  kutoka makao makuu ya DCI, wakisaidiwa na wataalam wa kiyasansi, wamechukua usukani wa kuchunguza chimbuko la mauaji ya Dkt. Mutiso.

 

Share This Article