Mwigizaji Winnie Bwire afariki

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji maarufu Winnie Bwire amefariki. Anaripotiwa kuaga dunia akiendelea kupokea matibabu ya saratani kwenye hospitali moja nchini Uturuki kulingana na familia yake.

Bwire amekuwa akiugua saratani ya matiti kwa miaka mitatu sasa.

Katika taarifa familia yake ilisema, ” Tunasikitika kutangaza kifo cha Winfred Bwire Ndubi ambaye alishindwa kwenye vita dhidi ya saratani leo Septemba 5 2024 wakati akitibiwa nchini Uturuki.”

Familia hiyo kadhalika ilishukuru wote ambao wamekuwa wakimsaidia Bwire akipambana na saratani.

Bwire amekuwa akiomba usaidizi wa kifedha mitandaoni ili kufanikisha matibabu. Alitangaza kwamba alihitaji shilingi milioni 5 za kugharamia matibabu na chakula nchini Uturuki.

Wakati moja mwigizaji huyo alilalamikia gharama ya juu ya matibabu akisema alikuwa ameshindwa na hali hiyo na kulazimika kuomba michango.

Atakumbukwa na wengi kutokana na uigizaji wake kwenye kipindi Sultana cha runinga ya Citizen ambapo aliigiza kama Dida.

Share This Article