Mwigizaji filamu maarufu Chuck Norris afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwigizaji filamu maarufu Chuck wa filamu kutoka nchini Marekani, Chuck Norris, ameaga dunia mapema leo akiwa na umri wa miaka 86.

Familia ya marehemu imetangaza kifo chake kupitia kwa kurasa za mitandao ya mwigizaji huyo.

Ingawa familia haijasema chanzo cha kifo, yamkini alifariki hospitalini akipokea matibabu.

Chuck Norris alitunga filamu kama vile The Hitman, The Delta Force, Delta Force 2, na The Colombian Connection.

Aidha, Norris alishirikishwa katika filamu za Missing in Action, Firewalker na Sidekicks, na alikuwa mwelekezi mkuu wa filamu ya Walker, Texas Ranger.

Pia Norris alishiriki mashindano kadhaa ya karate kati ya mwaka 1964 na 1974 alipostaafu.

Share This Article