Mwanasiasa wa upinzani DRC Cherubim Okende auawa

Dismas Otuke
1 Min Read

Mmoja wa viongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemkokrasia ya Congo, DRC Cherubin Okende amepatikana ameuawa kwa kupigwa risasi.

Mwili wa Chérubin Okende ulipatikana ndani ya gari katika mji mkuu wa Kinsasha ukiwa na majeraha ya risasi.

Okende alikuwa Waziri wa Uchukuzi serikalini kabla ya kujiuzulu mwezi Disemba mwaka jana na kujiunga na chama cha upinzani Ensemble pour la République chake Moïse Katumbi.

Baadaye, aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa chama.

Joto la kisiasa limepanda katika Jamhuri ya Kidemkokrasia ya Congo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *