Maafisa wa polisi katika wilaya ya Amuru nchini Uganda, wanamzuilia mwanamume wa umri wa miaka 20 kwa jina Oyet Sunday kwa madai ya kumbaka ajuza wa umri wa miaka 80.
Kulingana na polisi, mshukiwa huyo alitekeleza uovu huo tarehe 20 mwezi huu baada ya kumfumania ajuza huyo nyumbani kwake.
Inasemekana mshukiwa aliingia nyumbani kwa mshukiwa na kumtisha mwathiriwa kuwa atamuua iwapo atapiga kamsa, na kisha akambaka na kumwacha na majeraha.
Ajuza huyo aliwaambia Majirani ambao walimwandama na kumkamata mshukiwa huyo.
Nguo za mshukiwa huyo zilipatikana zikiwa na matone ya damu ambayo yanafanyiwa uchunguzi wa DNA.
Wakati huo huo maafisa wa polisi nchini Uganda wanawatafuta Wanachama wa genge la watu 15, waliombaka mwanamke wa umri wa miaka 23.
Kulingana na taarifa ya polisi, mwanamke huyo alihadaiwa na binamu zake wawili, waliombaka pamoja na watu wengine 13.
Polisi wanawatafuta washukiwa hao