Mwanamume afungwa miaka 25 kwa kumdhulumu na kumuua mtoto

Anadaiwa kutekeleza uovu huo usiku wa tarehe 18 mwezi Februari mwaka 2017, nyumbani kwa wazazi wa msichana huyo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamume afungwa miaka 25 kwa kumdhulumu na kumuua mtoto.

Mwanamume mwenye umri wa miaka 42 kutoka kaunti ya Meru, amehukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kumdhulumu kimapenzi na kumuua mtoto mwenye umri wa miaka 12.

Anadaiwa kutekeleza uovu huo usiku wa tarehe 18 mwezi Februari mwaka 2017, nyumbani kwa wazazi wa msichana huyo.

Mahakama ilifahamishwa kuwa, mshtakiwa huyo alikiri kutekeleza mauaji hayo, kama hatua ya kulipiza kisasi, baada ya kukataliwa kimapenzi na dada mkubwa wa mwathiriwa mwaka 2017.

Kesi hiyo ilikuwa imesitishwa baada ya mashahidi wote na wana familia wa mwathiriwa kuhama na wasijulikane waliko.

Kifungo hicho cha miaka 25 gerezani, kinahitimisha swala ambalo  limekaa takriban miaka tisa bila kusuluhishwa.

Justice Heston Nyaga, alipongeza Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kwa juhudi zao zilizofanikisha kukamilishwa kwa kesi hiyo.

Share This Article