Kenya na Austria zaimarisha uhusiano

Nchi hizo mbili zinashirikiana katika kubuni nafasi za ajira ughaibuni, na katika nyanja kama vile nishati mbadala, kilimo na teknolojia.

Martin Mwanje
1 Min Read

Kenya imeimarisha uhusiano wa kidiplomasia na biashara na Austria kwa kuhamasisha ushirikiano wa pande mbili. 

Rais William Ruto amesema nchi hizo zimeimarisha uhusiano katika kubuni nafasi za ajira ughaibuni, nishati mbadala, kilimo na teknolojia.

“Tunaishukuru Austria kwa kuajiri wauguzi 100 kutoka Kenya, idadi ambayo tunadhamiria kuongeza kupitia mafunzo ya lugha za kigeni katika Vyuo vya Mafunzo ya Matibabu nchini Kenya, KMTC,” alisema Ruto.

Aliyasema hayo alipomwaga Balozi wa Austria nchini Kenya Christian Fellner.

Balozi huyo amehudumu kwenye wadhifa huo nchini kwa kipindi cha miaka 8 iliyopita.

 

Share This Article