Shirikisho la soka Duniani, FIFA limesherehekea idadi ya mashabiki milioni 50 waliohudhuiaria fainali za Kombe la Dunia tangu kuanza kwa kipute hicho mwaka 1930.
Idadi hiyo ya mashabiki iliafikiwa wakati wa mechi ya raundi ya 16 bora Jumatatu jioni kati ya Uhispania na majirani wao Ureno katika uwanja wa Dallas.
Mashabiki 6,138,848 wamefika viwanjani kutazama mechi za Kombe la Dunia mwaka huu katika mechi 94 zilizochezwa, ikiwa wastani wa mashabiki 65,307 kwa kila mchuano.