6 wafariki kwenye ajali barabara kuu ya Nairobi-Mombasa

Watu wengine 41 walijeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyohusisha basi la Tahmeed na matrela mawili. Majeruhi wanatibiwa katika hospitali ya Machakos Level 5.

Martin Mwanje
1 Min Read

Watu 6 walifariki kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea leo Jumanne katika eneo la Kapiti, Konza kwenye barabara kuu ya Nairobi kuelekea Mombasa.

Watu wengine 41 walijeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyohusisha basi la Tahmeed na matrela mawili.

Majeruhi walikimbizwa katika hsopitali ya Machakos Level 5 ili kupata matibabu.

Akizingumza katika eneo la ajali, OCPD wa Kalama Patrick Gaithirira alithibitisha vifo vya watu hao sita na kutoa wito kwa madereva kuwa waangalifu barabarani.

Kwa upande wake, akizungumza katika hospitali ya Machakos Level 5, Waziri wa Afya wa kaunti ya Machakos Justus Kasivu alithibitisha kuwa majeruhi wanatibiwa hospitalini hapo na hali yao inaendelea kuimarika.

Aliongeza kuwa serikali ya kaunti hiyo inatoa usaidizi kwa familia zilizoathiriwa.

Share This Article