Kenya na Kazakhstan zatia saini mikataba ya makubaliano

Mikataba hiyo inajumuisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), huduma za serikali kupitia mtandaoni, uchukuzi na miundombinu, fedha, utalii, mabadiliko ya tabianchi, madini na teknolojia ya angani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya na Kazakhstan zatia saini mikataba ya makubaliano.

Kenya na Kazakhstan zimetia saini mikataba ya makubaliano kwa lengo la kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya  nchi hizo mbili.

Rais William Ruto ambaye yuko kwenye ziara ya kiserikali ya siku mbili katika taifa hilo la bara Asia, alisema mikataba hiyo inajumuisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), huduma za serikali kupitia mtandaoni, uchukuzi na miundombinu, fedha, utalii, mabadiliko ya tabianchi, madini na teknolojia ya angani.

“Lengo letu kuu ni kuhakikisha ukuaji wa ushirikiano unafanikisha manufaa kwa raia wa nchi hizo mbili,” alisema Rais Ruto.

Awali, Rais Ruto alihudhuria makaribisho ya taadhima katika kasri huru ya Astana nchini Kazakhstan, ambapo alisema uhusiano kati ya Kenya na Kazakhstan ulianza wakati yeye na Rais wa nchi hiyo Kassym-Jomart Tokayev walipokutana jijini New York nchini Marekani.

Kiongozi wa taifa ambaye ameandamana na mama wa taifa Rachel Ruto, alikariri kwamba biashara kati ya Kenya na Kazakhstan tayari imenanawiri katika sekta za majani chai, maua, mbolea na vifaa huku kukiwa na usafiri wa angani wa moja kwa moja baina ya Nairobi na Astana pamoja na mataifa mengine ya Asia ya Kati.

Share This Article