Adan Mohamed aapishwa kama Kamishna Mkuu wa KRA

Martin Mwanje
1 Min Read

Waziri wa zamani wa Viwanda Adan Mohamed ameapishwa leo Jumatano kuhudumu kama Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini, KRA. 

Hii ni baada ya Mohamed kuteuliwa na Waziri wa Fedha John Mbadi kuhudumu kwenye wadhifa huo kupitia gazeti rasmi la serikali la Mei 18.

Mohamed anajaza pengo lililoachwa na Humphrey Wattanga ambaye aliteuliwa na Rais William Ruto kuwa Balozi wa Kenya nchini Afrika Kusini.

Nadhari sasa itamwangazia Waziri huyo wa zamani kuona mbinu atakazotumia kukusanya mapato yanayohitajika mno na serikali ili kutekeleza miradi muhimu ya miundombinu nchini.

 

 

 

Share This Article