Shirikisho la kandanda nchini (FKF), limeanza majadiliano na Baraza na Magavana nchini (COG), kuhusu ushirikiano wa kupiga jeki soka ya mashinani katika kaunti zote 47 nchini.
Haya yalibainika baada ya kinara wa FKF Hussein Mohamed, kukutana na Mwenyekiti wa COG Ahmed Abdullahi Jumanne.
Akiwahutubia Wanahabari baada ya majadiliano hayo Abdullahi ambaye pia ni Gavana wa Wajir, alisema watasaini mkataba ndani ya siku 30 zijazo.
Alifichua kuwa mkatba huo utakuwa wa ushirikiano katika juhudi za kukuza soka ya mashinani ikiwemo marefa,makocha na uendeshaji ligi za kuanti.

Hussein Mahamed alisema wanatarajia ufadhili huo utachangia pakubwa katika makuzi ya vipaji kote nchini.
Mkataba huo punde utakaposainiwa pia utajumuisha mikakati ya kaunti kuelekea kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika AFCPON mwaka ujao.
Endapo utatiwa saini mkataba huo utakuwa wa kwanza na wa kipekee nchini huku ukitarajiwa kubuni fursa ukuzaji vipawa vya soka nchini.