Uchaguzi Mkuu ujao utakuwa wa haki na amani, asema Mudavadi

Mudavadi alitoa wito kwa wakazi wa Magharibi mwa nchi kukumbatia amani, umoja na mshikamano, taifa hili linapojiandaa kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2027.

Tom Mathinji
1 Min Read
Musalia Mudavadi - Mkuu wa Mawaziri wa Kenya.

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, utakuwa huru, haki na wenye amani.

Akizungumza Jumamosi katika kaunti ya Vihiga, Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, alipuuzilia mbali madai ya upande wa upinzani kwamba uchaguzi huo utakumbwa na ghasia.

“Tuna katiba moja ambayo inamhakikishia kila Mkenya haki ya kupiga kura. Wale ambao wanapigia debe migawanyiko na kueneza ukabila ni adui wa maendeleo,” alisema Mudavadi.

Mudavadi alitoa wito kwa wakazi wa Magharibi mwa nchi kukumbatia amani, umoja na mshikamano, taifa hili linapojiandaa kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2027.

“Uchaguzi wa amani utawezesha taifa hili kuangazia maendeleo, kubuni nafasi za ajira na kuimarisha maisha ya Wakenya wote,” alidokeza waziri huyo.

Alisema propaganda husababisha uharibifu kwenye maendeleo yanayoshuhudiwa katika eneo hilo, akiwataka wakazi wa eneo hilo kuhakikisha Rais William Ruto anashinda muhula wa pili.

Share This Article