Bafana Bafana yaicharaza Harambee Stars mabao 2-1 nyumbani

Timu hizo mbili zilipimana nguvu Jumanne usiku katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Bafana Bafana yaishinda Harambee Stars mabao 2-1 katika uwanja wa Nyayo.

Timu ya Taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, imekosa fursa ya kuandikisha ushindi katika mechi za kufuzu kwa michuano ya Mataifa bingwa Afrika 2027, baada ya kushindwa na Afrika Kusini mabao 2-1.

Timu hizo mbili zilipimana nguvu Jumanne usiku katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Relebohile Mofokeng alifunga mabao mawili katika dakika ya 68 na 86, na kuihakikishia bafana bafana ushindi, huku ikichupa hadi kileleni mwa kundi D.

Hata hivyo, Kenya ilijikakamua na kujipatia bao la kufuta machozi mnamo dakika ya 89, kupitia Mohammed Bajaber.

Ushindi huo wa Afrika Kusini unajiri siku nne baada ya timu hizo kuto sare ya mabao 2-2  kwenye mechi ya kusisimua iliyochezwa Jijini Johannesburg, Kenya ikitoka nyuma mara mbili na kupata mabao kupitia Michael Olunga na Ryan Ogam.

Share This Article