Mwanaharakati Morara Kebaso aachiliwa huru kwa dhamana ya 50,000

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwanaharakati Morara Kebaso ameachiliwa  huru kwa dhamana ya shilingi elfu 50 baada ya kukamatwa na polisi na kulala korokoroni jana usiku.

Kebaso alishtakiwa kwa kueneza uvumi na habari za uongo kuhusu Rais William Ruto.

Mawakili wa upande wa mlalamishi wamesema habari alizochapisha Kebaso ni uhalifu wa mtandaoni na ulilenga  kumchafulia sifa Rais Ruto.

Kesi hiyo itaamuliwa na mahakama tarehe 4 mwezi huu iwapo mashtaka yaliyowasilishwa  na kiongozi wa mashtaka yatatosha kuendeleza kesi hiyo.

Hii ni baada ya mawakili wa mwanaharakati huyo kukataa kula kiapo kujitetea.

 

TAGGED:
Share This Article