Washukiwa wa wizi wakamatwa Nyahururu

Wanaume hao wawili walipatikana wakiwa na mali inayoshukiwa kuibwa ya thamani ya shilingi laki 6.

Marion Bosire and Lydia Mwangi
1 Min Read

Maafisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Nyahururu wamekamata wanaume wawili wakiwa na mali inayoshukiwa kuibwa ya thamani ya shilingi laki 6.

Kulingana na naibu Kamishna wa eneo la Nyahururu Joseph Nyongesa, mali iliyopatikana inajumuisha simu za rununu, mitungi ya gesi, pikipiki, baiskeli kadhaa, vileo ghali na bidhaa za kielektroniki.

Nyongesa aliongeza kusema kwamba washukiwa hao wawili watafikishwa mahakamani kesho, huku polisi wakisaka washukiwa zaidi ambao hawajulikani waliko.

Wananchi kadhaa walifika katika kituo hicho cha polisi ambapo wengi waliweza kutambua mali zao zilizopotea.

Polisi wanaamini kwamba washukiwa hao ni wahalifu sugu ambao wana historia ya kutekeleza visa mbali mbali vya uhalifu katika maeneo ya Nyahururu na Ndaragwa.

Website |  + posts
Share This Article