Mwaka 2023 ulikuwa wa ufanisi mkubwa kwa wanariadha wa Kenya asema Korir

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwenyekiti wa chama cha Riadha Kenya kaunti ya Nairobi Baranaba Korir amesema mwaka 2023 ulikuwa wenye ufanisi mkubwa wa kiwango cha asilimia 80 kwa wanariadha wa Kenya.

Kwenye mahijiano ya kipekee na meza ya michezo KBC Korir, ametaja baadhi ya matukio makuu ya mwaka 2023 kama vile Faith Kipyegon kuvunja rekodi tatu za dunia ndani ya mwezi mmoja,Kelvin Kiptum kuvunja rekodi ya rekodi ya marathon iliyokuwa ikishikiliwa na Eliud Kipchoge.

Korir pia amesema kuwa wanariadha wa Kenya walijizatiti katika mashindano ya Riadha duniani mjini bUdapest  licha ya ushindani mkali.

YouTube player

Korir ambaye pia ni mwanachama wa baraza kuu la chama cha Riadha Kenya ameipongeza serikali kwa kuwasaidia na kufadhili miradi mbali mbali ya AK kama vile kambi za wanariadha chipukizi.

 

Share This Article