Makabiliano ya Ligi Kuu Kenya kuingia mzunguko wa 19

Dismas Otuke
1 Min Read

Kinyang’anyiro cha ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya kitaendelea mwishoni mwa juma hili kwa jumla ya mechi nane.

FC Talanta watakunjua jamvi la Jumamosi kwa kuwaalika Mathare United saa saba adhuhuri katika uga wa Dandora, kabla ya kuwapisha Kakamega Homeboyz watakaowaalika Mara Sugar kiwarani Mumias Complex, saa tisa na hatimaye mabingwa watetezi Gor Mahia wamenyane na matarishi Posta Rangers saa kumi jioni uwanjani Dandora.

Jumapili mikwangurano mitano itagaragazwa Maafande Kenya Police, wakishuka katika uchanjaa wa Machakos saa saba dhidi ya Batoto Ba Mungu, Sofapaka.

Kariobangi Sharks watakuwa ziarani Gusii dhidi ya Shaba FC saa nane, wakati Muranga’ Seal ikiwa mwenyeji wa Bandari FC saa tisa katika uwanja wa Sportpesa.

AFC Leopards itakabiliana na Nairobi City Stars kiwanjani Dandora, saa tisa kisha KCB wahitimishe ratiba kwa kuwatembelea Tusker FC, mechi iking’oa nanga saa kumi alasiri katika kiwara cha Machakos.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *