Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imetangaza kuwa mvua ya Niño inatarajiwa kuanzia wiki ijayo na itaendelea hadi mwezi Disemba.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Edward Muriuki amesema tayari kaunti zipatazo 24 zimeanza kushuhudia mvua, zikiwemo za maeneo ya Pwani, Magharibi na Bonde la Ufa.
Aliongeza kuwa kaunti nyinginezo zinatarajia mvua ndani ya wiki moja hadi mbili zijazo.
Kaunti ambazo tayari zinapokea mvua ni: Nandi, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Siaya, Busia, Baringo, Nakuru na Trans Nzoia.
Zingine ni Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet, West Pokot, Kisii, Nyamira, Kericho, Bomet, Kisumu, Homa Bay, Migori na Narok.
Maeneo ya Pwani yanayoshuhudia mvua ni Mombasa, Kwale, Lamu and Kilifi na Tana Delta.
Pia Marsabit, Mandera, Wajir, Garissa na Isiolo zinatarajia mvua kuanzia wiki ya pili ya mwezi huu.
Aidha, licha ya maeneo mengine kupokea mvua kubwa, baadhi yanatarajia viwango vya chini vya mvua.