Harambee Stars wako Kigali mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Rwanda

Pambano hilo la kujipima nguvu litasakatwa Jumatatu kuanzia saa moja usiku katika uwanja wa Amahoro.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars, imeendeleza mazoezi yake Jumapili mjini Kigali kujiandaa kwa mchuano wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji Rwanda Jumatatu usiku.

Stars waliekea Rwanda baada ya kutoka Guinea walikolazwa bao moja kwa bila na wenyeji katika mchuano wa pili wa kundi D kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON mwakani.

Pambano hilo la kujipima nguvu litasakatwa Jumatatu kuanzia saa moja usiku katika uwanja wa Amahoro.

Kenya inaorodheshwa ya 109 huku Rwanda ikishikilia nafasi ya 128 katika msimamo wa FIFA.

 

 

Share This Article