Mvua kubwa yatarajiwa nchini yaonya idara ya hali ya hewa

Dismas Otuke
1 Min Read

Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya inafuatilia kwa karibu dhoruba ya tropiki Ialy, ambayo kwa sasa iko Kusini-Magharibi mwa Bahari ya Hindi.

Dhoruba hiyo inatarajiwa kuongeza mvua katika maeneo ya magharibi mwa nchi na sehemu za nyanda za juu, mashariki mwa Bonde la Ufa, ikiwa ni pamoja na jiji kuu la Nairobi.

Wananchi katika maeneo hayo wamehimizwa kuendelea kupata taarifa na kujiandaa kukabiliana na mafuriko na majanga mengine yatokanayo na mvua kubwa.

Mawimbi makubwa pia yanatarajiwa juu ya bahari ya Hindi, huku upepo mkali wa kusini ukitarajiwa katika sehemu ya mashariki ya nchi.

Mvua kubwa itakayoshuhudiwa pwani ya Kenya inaweza kuenea katika maeneo mengine ndani ya nchi.

Idara ya hali ya hewa imesema itaendelea kufuatilia hali hiyo na kutoa mwongozo panapohitajika.

Share This Article