Maelfu ya raia wa Austria waliwasha mishumaa Jumanne usiku, kuwaomboleza waathiriwa wa ule mkasa ambapo watu 10 walifariki baada ya kufyetuliwa risasi katika shule moja.
Maafisa wa polisi walisema mshukiwa wa shambulizi hilo mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni mwanafunzi wa zamani wa shule hilo, alijitoa uhai ndani ya bafu, muda mfupi baada ya kutekeleza shambulizi hilo siku ya Jumanne.
Shambulizi hilo ambalo limetajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya hivi karibuni ya taifa hilo, lilitekelezwa katika shule ya upili ya Dreierschützengasse secondary, Kaskazini Magharibi mwa mji huo.
Watu 12 zaidi walijeruhiwa, huku lengo kuu la mshambuliaji huyo likiwa halijulikani.