Mvua kubwa yatarajiwa maeneo kadhaa nchini Jumatatu

Dismas Otuke
1 Min Read

Mvua kubwa inatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria ,bonde la ufa na Nairobi kwa mjibu wa ripoti kutoka kwa idara ya utabiri wa hali ya anga nchini.

Idara hiyo imeongeza kuwa mvua ya kiwango cha milimita 30 imeshuhudiwa nchini kwa kipindi cha saa 24 zilizopita huku viwango hivyo vikitarajiwa kupungua siku ya Jumatano lakini kuongezeka kuanzia Mei 22 katika ukanda wa pwani.

Kauntio zinazotarajiwa kushuhudia mvua kubwa ni pamoja na Kisumu, Homabay, Siaya, Migori, Busia, Kisii, Nyamira, Nandi, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Narok, Baringo, Nakuru, Trans-Nzoia , Uasin Gishu ,

na Elgeyo-Marakwet.

Kaunti nyingine ni West-Pokot, Turkana, Samburu, Nyandarua, Laikipia, Nyeri, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Nairobi, Machakos, Kajiado, Mombasa, Tana-River, Kilifi, Lamu na Kwale.

Idara ya utabiri wa hewa nchini imewashauri wananchi kutahadhari dhidi ya mafuriko katika maeneo mbali mbali.

Share This Article