Murkomen: Kikosi maalum kitabuniwa kukabiliana na ulanguzi wa binadamu

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, amesema serikali imeimarisha juhudi zake za kukabiliana na ulanguzi wa binadamu.

Kufuatia ufichuzi kwamba raia wengi wa Kenya wanasafirishwa katika mataifa ya ng’ambo kwa kazi za lazima na utumwa, waziri huyo alidokeza kuwa swala hilo linahitaji kuangamizwa kikamilifu.

“Kama wizara, tumeimarisha vita dhidi ya ulanguzi wa binadamu na tunalenga kubuni kikosi maalum kitachaokabiliana na uovu huo,” alisema Murkomen.

Hatua hii itahakikisha kutekelezwa kwa sheria kali za uhamiaji hasaa dhidi ya wale wanaotoa ahadi kwa vijana wetu kuhusu ajira bora ughaibuni,” alisema Murkomen.

Murkomen alikuwa akijibu maswala kwa kamati ya bunge la taifa kuhusu utawala wa taifa na Usalama wa ndani inayoongozwa na mbunge wa Narok Magharibi Gabriel Tongoyo.

Murkomen pia alifahamisha kamati hiyo kuwa serikali imebuni mikakati makhsusi kuhakikisha mizozo inatatuliwa kisheria kunapotokea sintofahamu, na hivyo kufanikisha amani miongoni mwa jamii.

Lengo la hatua hyo kulingana na waziri huyo, ni kuboresha uhusiano kati ya asasi za utekelezaji sheria na jamii.

Website |  + posts
Share This Article