Geofrey Muriira ni mmoja wa watu watatu waliopendekezwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukadiriaji Ubora wa Bidhaa Nchini, KEBS.
KEBS imependekeza majina matatu ya wanaowania kazi hiyo akiwemo Muriira ambaye kabla ya kusimamishwa kazi, alikuwa Mkurugenzi wa Ukadiriaji wa Ubora na Ukaguzi.
Muriira ni miongoni mwa maafisa 27 wa serikali waliosimamishwa kazi na Rais William Ruto mwezi Mei, kutokana na kutoweka kwa kwa magunia 20,000 ya sukari iliyoharibika.
Muriira alimaliza wa tatu kwenye usaili wa Mkurugenzi Mkuu nyuma ya Moses Sudi Oto na kaimu Mkurugenzi Mkuu Esther Ngari, waliomaliza katika nafasi za kwanza na pili mtawalia.