Marekani inakaribia kufunga mlango wake karibu nusu kwa Afrika

KBC Digital
5 Min Read

Marekani imenyanyua tena “upanga wake wa viza”, safari hii ukielekea kwa nguvu zaidi Afrika. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani vinavyoanika nyaraka za serikali, Rais Donald Trump anapanga kuongeza orodha ya nchi zinazopigwa marafuku raia wake kuingia Marekani katika wiki kadhaa zijazo.

Kati ya nchi 36 mpya, 26 ziko barani Afrika! Pamoja na orodha iliyotangazwa mapema mwezi huu, raia wa nchi 36 kati ya nchi 54 za Afrika watakabiliwa na marufuku kamili au nusu kuingia Marekani. Afrika, bara linalochukuliwa kama “bara lenye matumaini”, linakaribia kuwa eneo kuu kabisa ambalo Marekani “itakataza kikamilifu”.

Sababu za Marekani? Ni za kusemasema tu

Katika kumbukumbu yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alizipa nchi hizo siku 60 za “kujirekebisha” ili kufikia “viwango”. Je, viwango ni vipi? Kumbukumbu hiyo haielezi wazi, lakini inataja sababu kadhaa za marufuku hiyo:

“kuunga mkono ugaidi”; vitambulisho visivyo vya kuaminika; rekodi za uhalifu zisizoweza kuthibitishwa; Uuzaji wa uraia kwa watu wasioishi katika nchi hizo; Kiwango cha juu cha wanaokaa Marekani bila viza; kutotoa ushirikiano wa kurudisha raia wanaofukuzwa Marekani, n.k

Ufumbuzi ni nini? Rubio “kwa ukarimu” amependekeza: Nchi hizo zinaweza kukubali kupokea raia wa nchi nyingine wanaofukuzwa na Marekani, au kuchukua nafasi ya “Nchi Salama ya Tatu” kupokea wahamiaji wanaotafuta hifadhi Marekani. Ajabu, mipango ya hila ya Marekani inaonekana hadi kuvuka bahari ya Atlantiki!

Wakati akitangaza orodha ya kwanza ya marufuku ya kuingia Marekani, Trump alitumia tukio la mashambulizi yaliyotokea jimboni Colorado akionyesha “hatari kubwa” ya “wageni wasiokaguliwa”. Lakini hali halisi ni kuwa mtuhumiwa alitoka Misri (nchi iliyoko kwenye orodha inayozingatiwa), lakini nchi aliyoishi Kuwait haiko kwenye orodha. Mantiki hiyo ya Marekani imeepuka kabisa na baadhi ya “mashirika”.

Wakosoaji wamesema wazi: Kutoka marufuku ya kuingia Marekani kwa raia wa nchi 7 hapo awali, hadi sasa nchi 26 mpya za Afrika, mara nyingi zinazolengwa ni nchi zenye watu weusi, zenye mapato ya chini. “Urithi” uliobatilishwa na Biden, Trump anaonekana kuwa anataka “kuurithi maradufu na kuuendeleza”!

Ni nani anayeathiriwa na kuuzwa zaidi?

Takwimu za Taasisi ya Sera za Uhamiaji Marekani zinaonyesha kuwa: kati ya wahamiaji milioni 44 Marekani, takriban milioni 2 wanatoka nchi za Afrika, nao ndio kikundi kinachokua kwa kasi zaidi hivi karibuni. Wengi wao wana shahada za juu, na ndio kikundi kikubwa zaidi cha wahamiaji kwenye soko la nguvu kazi Marekani. Nigeria, Ethiopia, Ghana, Misri… nchi hizi zilizopo kwenye “orodha inayozingatiwa”, ndizo zimepeleka watu wenye ujuzi zaidi Marekani. Wataalamu wanaonya: marufuku hiyo ikitekelezwa, kwa raia wa Afrika ambao hawajapata uraia wa Marekani itakuwa ni kama “amri ya kuwashika” – kuondoka kwao Marekani kunaweza kumaanisha kushindwa kurudi tena, na familia zitavunjika.

Kwa Marekani, sio tu itapoteza mawasiliano ya watu, bali pia fursa kubwa za ushirikiano.

Mkurugenzi wa Mradi wa Dunia ya Kusini katika Taasisi ya Washauri Bingwa ya Quincy Marekani Sarang Shidore ametoa onyo kali kuwa marufuku ya viza ni kama “kujenga ukuta”. Anaikumbusha Marekani kuwa “Afrika ni muhimu sana kwa Marekani kwa sababu ina maliasili nyingi, masoko yanayokua na idadi kubwa ya watu wenye vipaji.” Je, Marekani inataka kukataza uhamiaji wa watu huku ikitawala peke yake masoko ya maliasili barani Afrika? Hakuna jambo zuri kama hilo duniani!

Kufunga mlango ni sawa na kupoteza siku zijazo

Kwa kutumia jina la “usalama” na “kufuata kanuni”, serikali ya Marekani inatumia marufuku ya viza kama silaha, lakini inachofanya kwa kweli ni “kujifungia ndani kama kwenye kuta” na kujidhuru wakati ikidhuru wengine. Inaharibu maisha na matumaini ya mamilioni ya watu wa kawaida, inasababisha kujitenga na bara lote la Afrika lenye uwezo mkubwa, na kuacha fursa ya ushirikiano wa watu wenye vipaji, masoko na maliasili muhimu.

Hata hivyo, athari mbaya zaidi ni kwamba, kutoka ushuru wa upande mmoja hadi vikwazo vya viza, ukuta inaojenga Marekani kwa kasi unaonyesha waziwazi kiburi, upendeleo na mawazo yake finyu, na kupeleka fursa kwa mikono yake miwili kwa wenzake ambao wanafungua milango yao na kuwatendea watu kwa usawa. Mapema mwezi huu, China ilitangaza kuondoa kabisa ushuru wa bidhaa kutoka nchi 53 za Afrika zenye uhusiano nao wa kidiplomasia, na kuonesha kwa vitendo namna ya kujenga pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika hali zote. Nchi za Afrika zinaona yote haya, na mioyoni mwao wana kipimo.

KBC Digital
+ posts
Share This Article