Multichoice yawarai Wakenya kuunga mkono sinema za humu nchini

Dismas Otuke
1 Min Read
Kushoto hadi kulia:Msimamizi wa vipindi MultiChoice Africa Holdings East, West and Southern Africa, Timothy Okwaro, Meneja wa uhusiano mwema MultiChoice Kenya, Elisha Kamau,Afisa wa Mipango tume ya filamu nchini , John Kyalo

Kampuni ya MultiChoice Kenya imewarai Wakenya kuunga mkono soinema na vipindi vya runinga vya humu nchini ili kukuza sanaa ya kenya.

Haya yalisemwa na Meneja mkurugenzi Mkuu wa kampuni  ya Multichoice Kenya Nzola Miranda, wakati wa onyesho la sinema za humu nchini katika mkahawa wa Windsor kaunti ya Nairobi.

“Tumejitolea kuendelea kuunga mkono talanta za Wakenya  kupitia sinema . Tumeona mabadiliko makubwa kuhusu matakwa ya  watazamaji wetu wa vipindi na sinema za humu nchini.Sinema zetu kadhaa zimetambulika katika tuzo mbalimbali kama vile Kalasha International TV ; Film Market Festival Awards.

Sinema za humu nchini ambazo zimetambulika kimataifa ni kama vile:- ‘Kam U Stay’ katika kitengo cha igizo bora kwa runinga, Zari,  “The Death of a Kenyan Heiress” miongoni mwa vingine.”

“Tumeona fursa kubwa ya kukuza sinema zetu za humu nchini  na hii ni kupitia kwa Wakenya kuunga mkono vipindi vya humu nchini.”akasema Miranda

Maonyesho hayo ya sinema na vipindi vya humu nchini huandaliwa mara kwa mara na kampuni ya Multichoice,  kwa lengo la kuwaleta pamoja waigizaji ,watayarishi na watamazaji wa sinema za humu chini.

Share This Article