Chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kwa sasa kinaongoza mazishi ya kaka ya mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu, Mzee Alute Mughwai Lissu.
Mazishi ya Mughwai yanaendelea nyumbani kwake katika kijiji cha Mahambe, Wilaya ya Ikungi eneo la Singida baada yake kufariki usiku wa kuamkia Novemna Mosi, 2026.
Familia iliamua kuahirisha mazishi ya kaka huyo mkubwa wa Tundu Lissu kusubiri hukumu yake kwenye kesi ya uhaini iliyokuwa ikimkabili, hukumu iliyotolewa Ijumaa Novemba 6, 2026.
Mwili wa mwendazake ulipelekwa jana kwenye makazi yake ya Arusha kabla ya kusafirishwa usiku hadi nyumbani kwa ajili ya mazishi.
Ni katika mkutano uliofanyika usiku nyumbani kwa Lissu ambapo familia iliamua kukabidhi uendeshaji wa mazishi kwa chama cha CHADEMA.
Naibu Katibu Mkuu wa chama ambaye anawakilisha eneo la Tanzania bara Aman Golugwa alichaguliwa mrakibu mkuu wa shughuli hiyo ambayo inaendela.
Akikubali jukumu hilo, Golugwa alihakikishia wote waliokuwa wakipanga kuhudhuria mazishi leo kuhusu shughuli nzuri ya amani ya kuaga mwendazake.
Golugwa alisema pia kwamba viongozi mbali mbali wa CHADEMA kutoka ote nchini Tanzania wangehudhuria mazishi ya leo.
Mwanamuziki na mwanachama wa chama hicho Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr. Sugu alichapisha picha inayomwonyesha akisaini kitabu cha rambirambi nyumbani kwa Mughwai.
“Mwenyekiti wetu Lissu alituambia tuje kumzika Mzee Alute Mughwai Lissu…Nami nimekuja kijijini Mahambe, Ikungi, Singida” aliandika Sugu.