Mudavadi: Serikali inaendelea kubuni mazingira bora kwa Wakenya ughaibuni

Mudavadi yuko Jijini Accra, Ghana kuhudhuria mkutano kuhusu ufadhili wa Umoja wa Mataifa.

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi ashiriki mazungumzo na Wakenya wanaoishi nchini Ghana.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesema serikali inaendelea kubuni mazingira mwafaka kwa Wakenya walio ughaibuni.

Akizungumza leo Ijumaa aliposhiriki mazungumzo na Wakenya wanaoishi na kufanya kazi nchini Ghana, Mudavadi aliwahimiza kuendelea kutoa mchango wao kwa ukuaji wa taifa hili, bila kuzingatia umbali waliko.

“Popote Wakenya wanedapo, wao hupeleka talanta na bidii ya taifa hili,” alisema Mudavadi.

Mudavadi aliyepia Waziri wa Mambo ya Nje, alidokeza kuwa Wakenya wanaoishi ughaibuni, huchochea ukuaji wa uchumi kwa kuunganisha biashara na kubuni fursa mpya kwa vijana wa taifa hili.

“Nilipowasili  Accra, Ghana,  nilizungumza na wataalam na wafanyabiashara kutoka Kenya, ambao wanatafuta riziki ughaibuni, lakini bado wanadumisha uhusiano dhabiti na nyumbani,” alisema Mudavadi.

Mudavadi yuko Jijini Accra, Ghana kuhudhuria mkutano kuhusu ufadhili wa Umoja wa Mataifa.

Share This Article