Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, amesema bidhaa nyingi za Kenya zinapaswa kufikia soko la kimataifa, uwekezaji kuimarika na nafasi zaidi za ajira kubuniwa kutoka na biashara kati ya Kenya na Marekani.
Mudavadi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, aliyasema hayo alipokutana na balozi wa Marekani hapa nchini Susan M. Burns Jijini Nairobi, ambapo walijadili kuhusu kupanua biashara, uwekezaji katika sekta ya kibinafsi na ubadilishanaji wa teknolojia.
” Nilipongeza kuongozwa muda kwa utekelezaji wa sheria ya AGOA hadi mwezi Disemba mwaka 2028,” alisema Mudavadi.
Aidha, alielezea kujitolea kwa Kenya kushiriki biashara ya muda mrefu na Marekani, ili kufanikisha bidhaa za Kenya kufikia soko la Marekani na kuchochea ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa hapa nchini.
“Kwa wakulima wetu, wauzaji bidhaa nje ya nchi na wabunifu, lengo ni kufikia masoko makubwa, kupanua biashara na kuhakikisha riziki endelevu,” aliongeza Mudavadi.