Idadi ya walioambukizwa Ebola yafika 9,000 DRC

Kulingana na wizara hiyo, visa 9,066 vimenakiliwa na watu 4,381 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 9,000 waambukizwa Ebola nchini DRC.

Wizara ya Afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imesema watu 9,000 kufikia sasa, wameambukizwa ugonjwa wa Ebola, huku taifa hilo likijizatiti kukabiliana na msambao wa ugonjwa huo hatari.

Kulingana na wizara hiyo, visa 9,066 vimenakiliwa na watu 4,381 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo.

Kwa sasa hakuna tiba ambayo imeidhinishwa kwa aina hiyo ya Bundibugyo, ambayo inazidi kuibua wasiwasi kuhusu maambukizi kwenye mipaka.

Juma lililopita Kenya ilinakili kisa cha kwanza cha ugonjwa huo wa Ebola, ambapo raia wa Kenya aliyekuwa nchini DRC, alisafiri kupitia Uganda kabla ya kuwasili Nairobi na kufariki.

Mapema mwaka huu, Uganda ilinakili visa 20 vya Ebola na vifo viwili, lakini taifa hilo litangaza halina ugonjwa wa Ebola mwezi Agosti.

TAGGED:
Share This Article