Mudavadi awasili China kwa ziara rasmi ya siku tatu

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi awasili nchini China.

Waziri mwenye mamlaka makuu aliyepia waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi, amewasili Jijini Beijing nchini China kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Capital Jijini Beijing, Mudavadi alilakiwa na Yu Yong na bi Xu Benin, ambao ni manaibu wakurugenzi wa maswala ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya China, pamoja na balozi wa Kenya nchini China Willy Bett.

Mudavadi ameandamana na katibu katika idara ya maswala ya bunge Aurelia Rono miongoni mwa maafisa wengine wa serikali.

“Mkutano huo unafuatilia mazungumzo yaliyotekelezwa muhimu kati ya Kenya na China hasaa kutokana na ziara ya hivi majuzi ya rais William Ruto nchini China,” ilisema afisi ya Mudavadi kupitia kwa taarifa.

Wakati wa ziara hiyo, waziri huyo mwenye mamlaka makuu, atashiriki mazungumzo na maafisa wakuu wa serikali ya China, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, uwekezaj, ajira na usalama kati ya Kenya na China.

“China inaendelea kuboresha ushirikiano wake na Kenya, huku ikiongoza katika kutekeleza miradi ya miundo msingi na kupiga jeki ukuaji wa sekta kadhaa za kiuchumi,” ilisema wizara hiyo.

Share This Article