Mtu mmoja afariki baada ya kimbunga kuathiri Ufilipino

Marion Bosire
1 Min Read

Mtu mmoja amethibitishwa kufariki baada ya kimbunga kwa jina Doksuri kuathiri upande wa kaskazini wa nchi ya Ufilipino.

Kimbunga hicho chenye upepo wa kasibya kilomita 175 kwa saa, kiling’oa paa za nyumba, kusababisha mafuriko na kukatiza nguvu za umeme.

Kimbunga Doksuri kilifika Ufilipino Jumatano na kinatarajiwa kuendelea kwa kasi ambayo kiko nayo kinapoelekea Taiwan na China baadaye wiki hii.

Afisi ya kushughulikia majanga nchini humo ilitangaza kifo cha mtu mmoja katika mkoa wa Rizal ambao uko upande wa mashariki wa mji mkuu Manila.

Mkoani Cagayan, zaidi ya watu elfu 12 walihamishwa kutoka makazi yao na makazi, shule na maeneo ya kazi yaliyo katika hatari ya mafuriko kufungwa.

Gavana wa Cayagan Manuel Mamba alizungumza na wanahabari kwa njia ya simu na kuthibitisha uharibifu mkubwa uliosababishwa na kimbunga Doksuri. Alisema baada ya kimbunga hicho, watafanya ukaguzi kufahamu kiwango cha uharibifu huo.

Mashamba ya mahindi na mpunga katika bonde la Cagayan ambayo awali yalikuwa yamekumbwa na kiangazi yanahofiwa kuharibiwa kabisa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *