Mshukiwa wa wizi wa kimabavu akamatwa Eldoret

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa wizi wa kimabavu akamatwa Eldoret.

Maafisa wa polisi wamemkamata mshukiwa wa wizi wa kimabavu, mjini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu.

Alikamatwa baada ya ripoti kupigwa kwenye kituo cha polisi cha Parklands Juni 28, 2025, kuhusu gari ambalo limekuwa likitumiwa kutekeleza uhalifu.

Mshukiwa huyo alipatikana na gari aina ya Toyota Axio, ambalo kwa sasa linazuiliwa na maafisa wa polisi.

Wakati maafisa wa usalama walipopekua gari hilo, walipata sare za polisi na nambari za usajili wa gari, ambazo zinashukiwa zimekuwa zikitumika wakati wa shughuli hizo wa uhalifu.

Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Parklands, huku uchunguzi ukiendelea.

Huduma ya Taifa ya polisi imepongeza juhudi za maafisa wa uchunguzi, huku ikihakikishia umma kujitolea kwake kufanikisha upatikanaji usalama na uzingatiaji sheria.

Website |  + posts
Share This Article