Maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI, wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati katika eneo la Lari, kwenye barabara kuu ya Nairobi-Nakuru.
Wakati wa operesheni hiyo iliyotekelezwa siku ya Jumatatu, maafisa hao walisimamisha gari aina ya Isuzu D-Max lenye nambari za usajili KBK 030J ambalo lilikuwa likiendehswa na Francis Kairu na baada ya upekuzi mihadarati hiyo ilipatikana.
Baadaye maafisa hao walimpeleka mshukiwa huyo pamoja na gari hilo hadi makao makuu ya DCI Jijini Nairobi, ambapo walipekua zaidi gari hilo na kupata vifurushi 80 vya mihadarati hiyo kwenye gari hilo.
Kupitia ukurasa wake wa X, idara ya DCI ilisema imejitolea kukabiliana vilivyo na uuzaji, usambazaji na utumizi wa mihadarati hapa nchini.