Polisi wa ujasusi kutoka kitengo cha mauaji jana Alhamisi walimkamata Kennedy Kalombotole, mshukiwa mkuu wa mauaji ya kinyama ya wagonjwa wawili waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta, KNH.
Kalombotole anashukiwa kumuua Edward Maingi Ndegwa Julai 11 mwaka huu katika wadi nambari saba ya hospitali hiyo.
Yamkini mshukiwa huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Kenyatta Disemba 1 mwaka 2024, na pia alishukiwa kuhusika katika mauaji mengine ya mgonjwa Gilbert Kinyua Muthoni aliyekuwa na umri wa miaka 40, baina ya usiku wa Februari 6 na 7 mwaka huu.
Katika muaji ya hivi punde, polisi walibaini kuwa mshukiwa aliingia katika wadi ya orofa ya saba alikokuwa amelazwa Maingi usiku wa manane na kumdunga kisu.
Kalombote yuko korokoroni akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashataka ya mauaji.
 
					 
			 
                                
                              
		 
		 
		 
		