Msemaji wa serikali: China haikuitaarifu Japani kabla ya jaribio la ICBM

Martin Mwanje
1 Min Read
Yoshimasa Hayashi - Msemaji wa serikali ya Japani

Msemaji wa serikali ya Japani Yoshimasa Hayashi amesema China haikuitaarifu Japani Japani kuwa itafanya jaribio la kombora la balistiki la kuvuka mabara, ICBM kabla ya kulirusha katika Bahari ya Pasifiki leo Jumatano. 

Hayashi aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari.

“Hapakuwa na notisi kutoka kwa upande wa China iliyotolewa mapema.” alisema Hayashi.

Wizara ya Ulinzi ya China imetangaza kuwa imerusha kombora la ICBM ambalo lilitua katika Bahari ya Pasifiki leo Jumatano.

Kulingana na wizara hiyo, kombora hilo lilibeba mfano wa kichwa cha kombora kwa kusudi la kufanya mazoezi.

Imeongeza kuwa urushaji huo uliendana na mpango wake wa mazoezi ya kila mwaka na kwamba ulifanywa kwa mujibu  wa sheria ya kimataifa.

Share This Article